UTARATIBU WA MAOMBI

SOMO MSTARI MAANDIKO
Utoaji mimba Zaburi 139:13-16 Yeremia 1:4-5 Maana wewe ndie ulie niumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana, Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilipo amriwa kabla hazijawa bado.

Unyanyapaa

Kutoka 22:21

1 Wakorinto. 9:18

Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya misri.

Kuwajibika

1 Wakorintho. 10:23-24

1 Wakorintho. 8:7-12

 Vitu vyote vinaruhusiwa, lakini si vitu vyote vina faida. `Vitu vyote ni halali,' lakini si vyote vinajenga. Mtu asita fute yale yanayomfaa yeye peke yake, bali atafute yale yanayomfaa jirani yake.

Mashtaka

Ufunuo. 12:10

Luka 6:7

 Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, ``Sasa umeti mia wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake yamefika. Kwa kuwa mshtaki wa ndugu zetu anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana ametupwa chini

Ujana

1 Timotheo 4:12

Mhubiri. 12:1

 Mtu asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe mfano mwema kwa waamini wote kwa maneno yako, kwa mwenendo wako, katika upendo, imani na usafi.

Kufanyika Mwana Kiroho

Waefeso 1:4-5

Mungu alituchagua sisi tuwe ndani ya Kristo hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na lawama mbele zake. Kwa upendo wake, alipanga kabla ya mambo yote, kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe;

Uzinzi

Kumb. 5:18

1 Wakorintho. 6:9

Waebrania. 13:4

Usizini. 1 Wakorinto. 6:9  Do you not know that the unrighteous will not inherit the kingdom of God? Do not be Je, hamjui kwamba wasio na haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike, waasherati hawataurithi Ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wapotoshaji;

Ushauri

Mithali 12:15

Mithali 19:20

Njia ya mpumbavu imenyooka machoni pake mwenyewe; Bali yeye alien a hekima husikiliza shauri. Mithali 19:20 Sikiliza mashauri, upokee mafindisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho

Upendo

Zaburi 42:1-2

1 Wakorintho. 7:3

Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji, Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shuku, Ee Mungu wangu. Nafsi yangu inamuonea kiu Mungu, Mungu alie hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?

Hasira

Waefeso 4:26-27

Wakolosai. 3:8 

Yakobo 1:19

Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima na kumpa shetani nafasi.

Kupotoka

1 Timotheo 4:1

Matendo 20:28-30

Roho anasema wazi wazi kwamba katika siku za mwisho watu wengine wataiacha imani yao na kusikiliza roho za udanganyifu na mafundisho ya mashetani.

Sura ya nje

1 Samueli 16:7

1 Wathesalonike. 5:22

Lakini bwana akamwambia Samweli, Usitazame uso wake, wala ulefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa.Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu hutazama sura ya nje, bali Bwana hutazama moyo,"

Mabishano

Wafilipi 2:14-15

Tito 3:10

Fanyeni mambo yote bila manung'uniko au mabishano ili msiwe na lawama au kosa bali muwe wana wa Mungu wasio na kasoro katika ulimwengu uliopotoka, mking'aa kama nyota angani,

Nuru

Warumi 13:12

Waefeso 6:11-18

Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Kwa hiyo tutupe kando matendo ya giza, tuvae silaha za nuru.

Matumaini

Waefeso 3:11-12

2 Timotheo 1:12

1 Yohana 5:11-13

Mpango huu ulikuwa sawasawa na mapenzi yake yaliyotimi zwa katika Kristo Yesu Bwana wetu, ambaye tukiwa ndani yake, tuna ujasiri na uhakika wa kumkaribia Mungu kwa njia ya imani katika Kristo.

Kutosadiki kuwa yuko Mungu

Zaburi 14:1

Warumi 1:20

 

Mpumbavu husema moyani, ‘’Hakuna Mungu.’’ Warumi 1:20  Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio.

 

Malipo ya dhhambi

Warumi 3:23-24

Warumi 5:11

kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo

Ushirika wa pamoja

Waebrania 10:23-25

Matendo 4:31

 Tushikilie kwa makini tumaini tunalokiri kwa maana yeye ali yeahidi ni mwaminifu. Na tujishughulishe kutafuta jinsi ya kuhimizana katika kuonyeshana upendo na kutenda mema. 25Tusiache kukutana pamoja, kama wengine wanavyofanya, bali tutiane moyo, hasa zaidi tunapoona siku ile ikikaribia.

Nia

Wafilipi 2:3-5

Msifanye jambo lo lote kwa ajili ya ubinafsi au kwa kujiona, bali kuweni wanyenyekevu, mkiwahesabu wengine kuwa bora kuliko ninyi. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu ajishughulishe pia kwa faida ya wengine. Muwe na nia kama ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu;

Mamlaka

Warumi 13:1-2

Waebrania 13:7,17

Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu.

Ubatizo

Warumi 6:3-8

Mathayo 28:18-20 Matendo 2:38-41

 

Na hata kama baadhi yao hawaku amini,je, kutokuamini kwao kutamfanya Mungu aache kuwa mwaminifu? Hata kidogo!Mungu ataendelea kuwa wa kweli hata kama kila mwan adamu atakuwa mwongo. Kama ilivyoandikwa katika Maandiko,``Wewe Mungu, uthibitishwe kuwa wahaki katika maneno yako, na mshindi katika hukumu.'' Lakini iwapo uovu wetu unadhihirisha wazi kwamba Mungu ni mwenye haki, tusemeje basi? Je, tuseme kuwa Mungu hana haki kutuadhibu? Hapa ninasema kibinadamu. La hasha! Mun gu ana haki kabisa kutughadhibikia! Kama sivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu? 7Mtu anaweza kusema,``Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha ukweli wa Mungu na hivyo kudhihirisha utukufu wake, kwa nini basi ninahukumiwa kama mwenye dhambi?'' Kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, ``Tutende maovu ili wema udhihirike''? Hakika hukumu wanayoipata ni ya haki.

Imani

Warumi 4:5

Yohana 3:16-18

Yohana 3:36

Lakini kwa mtu ambaye hakufanya kazi ila amemtegemea Mungu anayewahesabia haki waovu, imani yake inahesabiwa kuwa haki.

Ukarimu

Isaya 58:7,10

Mithali. 19:17, 21:13

Je! Sio kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje ya nyumba yako? Umwonapo mtu alie uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapo pambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita na Bwana ataitika; naye atasema, mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyo teswa; ndipo nuru yako itakapo pambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.

Bibilia

Waebrania 4:12

2 Petro 1:20-21

Kwa maana neno la Mungu ni hai tena lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili, linachoma kabisa na kutenganisha nafsi na roho, viungo vya mwili na mafuta yaliyomo ndani yake; na kutambua nia na mawazo ya mioyo ya watu.

Kukufuru

Mathayo 12:31-32

Mathayo 15:19 

Wakolosai 3:8

nawaambieni, watu watasamehewa kila aina ya dhambi na kufuru lakini mtu ata kayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. ``Na mtu atakayesema neno kumpinga Mwana wa Adamu ata samehewa, lakini ye yote atakayempinga Roho Mtakatifu hatasame hewa, katika ulimwengu huu wala katika ulimwengu ujao.''

 

Baraka

Waefeso 1:3

Zaburi 24:25

Waebrania 6:7

Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya Kristo.

Damu

Waebrania 9:22

1 Petro 1:18 

Matendo 20:28

Waefeso 1:7

 Hakika katika sheria, karibu kila kitu hutakaswa kwa damu; na pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi.

Mwili wa Kristo

1 Wakorintho12:12-13,27

Kama vile mwili ulivyo mmoja lakini una viungo vingi, na viungo vyote ingawa ni vingi vinafanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo na Kristo. Kwa maana tumebatizwa na Roho mmoja katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wagiriki, kama ni watumwa au watu huru; nasi tumepewa tunywe, huyo Roho mmoja. Basi ninyi ni mwili wa Kristo, na kila mmoja wenu ni kiungo cha huo mwili

Kitabu cha Uzima

Ufunuo 3:5

Wafilipi 4:3

Ufunuo 20:15

Atakayeshinda atavikwa vazi jeupe kama wao, nami sitafuta jina lake katika kitabu cha uzima bali nitalikiri jina lake mbele ya Baba yangu na mbele za malaika wake.

Kuzaliwa mara ya pili

1 Petro 1:22-23

Yohana 3:3-8

1 Yohana 3:9,4:7,

5:1,4

Na sasa kwa kuwa mmekwisha kujitakasa kwa kuitii ile kweli na kuwapenda ndugu zenu kwa kweli, pendaneni kwa moyo wote. 23Maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa mbegu isiyoharibika, kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu hata milele.

Biashara

Waefeso 6:6-7    Luka 2:49 

Matendo 6:3

1 Wathesalonike 4:11

 Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu.

Kutenda Mema

Isaya 1:17

Luka 14:13-14

Jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake, mteteeni mjane. Luka 14:13-14 - .

Tamaa za mwili

Mathayo 6:19-21

1Yohana 2:15-17

1 Timotheo 5:6

2 Timotheo 3:4 

Yakobo 5:5

.Msijiwekee mali nyingi duniani ambapo wadudu na kutu huharibu na wezi huvunja na kuiba. Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba. Kwa sababu pale akiba yako ilipo ndipo moyo wako uta kapokuwa.''

Useja/ Ujane

Matayo 19:10-12

1 Wakorintho 7:8,9,28

1 Timotheo 4:1-3

 Wanafunzi wake wakamwambia, ``Kama hivi ndivyo hali ilivyo kati ya mume na mke, basi ni afadhali mtu asioe!'' Yesu akajibu, ``Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya isipokuwa wale ambao Mungu amewajalia Kwa maana wako watu wasioweza kuoa kwa sababu wamezaliwa na hali hiyo; na wengine wamefanywa hali hiyo na binadamu; na pia wako wengine ambao wameamua kutokuoa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye kuli pokea fundisho hili na alipokee.''

Sifa

Mathayo 5:3-8

2 Petro 1:4-9

Wamebarikiwa walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbin guni ni wao. Wamebarikiwa wanaoomboleza; maana watafarijiwa. Wamebarikiwa walio wapole; maana watairithi nchi. Wamebari kiwa wenye hamu ya kutenda haki; maana wataridhishwa. Wamebari kiwa walio na huruma; maana nao watahurumiwa. Wamebarikiwa walio na moyo safi; maana watamwona Mungu. Wamebarikiwa walio wapatanishi; maana wataitwa wana wa Mungu. 10Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.

Utakatifu

1 Wakorintho 6:19-20 

1 Timotheo 4:12

Hamjui kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu anayekaa ndani yenu, ambaye mme pewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe; 20mmenunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Watoto

Kumb. 6:5-9

Zaburi 127:3-5

Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote. Na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo na upndokapo.

Chagua

Yoshua 24:15

Mathayo 6:24

Mithali 12:26

 

Ninyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo yam to, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; Lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

Kanisa

Waefeso 2:19-20

Mathayo 16:18

Waefeso 5:25

Kwa hiyo, ninyi sasa siyo wageni tena wala wapita njia, bali mmekuwa raia halisi pamoja na watu wa Mungu na familia ya Mungu. Ninyi mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni.

Mavazi

1 Timotheo 2:9-10

1 Petro< 3:3-5

Kumb.< 22:5

Kadhalika, nataka wanawake wajipambe kwa heshima na kwa busara. Mavazi yao yawe nadhifu, si kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu na mavazi ya gharama kubwa, 10bali kwa matendo mema kama iwapa savyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.

Faraja

Yohana 16:33

Zaburi 34:17-18

2 Wakorintho 1:3-4

Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.''

Manung’uniko

Zaburi 142:1-2

1 Wakorintho 10:6-10

Kwa sauti nitamlilia Bwana, kwa sauti yangu nita mwomba Bwana dua. Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, shida yangu nitaitangaza mbele ya Bwana.

Mapatano

2 Wakorintho 6:14-17

 Msiambatane pamoja na watu wasioamini. Kwa maana kuna uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? Kuna kuelewana gani kati ya Kristo na shetani? Mwamini ana uhusiano gani na asiyeamini? Kuna uelewano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema, ``Nitaishi ndani yao na kutembea kati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkajitenge nao, asema Bwana. Msiguse cho chote kisicho safi; ndipo nitawakaribisha kwangu. Nami nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa vijana wangu na binti zangu, asema Bwana Mwenyezi.''

Toba

Zaburi 32:5

Zaburi 51:3

1 Yohana 1:7-10

Nilikujulisha ndambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nikasema, nitayakiri maasi yangu kwa BWANA. Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.

Dhamiri

1 Timotheo1:18-19

1 Timotheo 1:5–4:2

Tito 1:15 

1 Timotheo 4:2

Mwanangu Timotheo, ninakukabidhi agizo hili, kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa juu yako, ili kwa kuyafuata uweze kupigana ile vita njema, ukishikilia imani na dhamiri njema. Watu wengine, kwa kukataa kuisikiliza dhamiri yao, wameangamiza imani yao.

Ushupavu

Yoshua 1:9

Mithali 28:1

Zaburi 31:24

Je! Si mimi niliye kuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifathaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

Agano

2 Wakorintho 3:5-6

1 Wakorintho 11:25

Haina maana kwamba sisi tunaweza wenyewe kupima cho chote tuna chofanya, lakini uwezo wetu unatoka kwa Mungu. Ni yeye ali yetuwezesha sisi kuwa wahudumu wa agano jipya, ambalo limefanywa, si kwa maandishi, bali kwa Roho. Kwa maana maandishi huleta kifo, lakini Roho huleta Uzima..

Uchoyo

Luka 12:15

Wakolosai 3:5-6

Ndipo akawaambia, ``Jihadharini na jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana uhai wa mtu hautokani na wingi wa mali aliyo nayo.'' Wakolosai.3:5-6 Basi, yaangamizeni kabisa mambo yote yanayotokana na asili yenu ya kidunia: uasherati, mawazo machafu, tamaa mbaya, nia mbaya na choyo ambayo ni ibada ya sanamu. Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja.

Uumbaji

Wakolosai 1:15-17

Mwanzo 1:1

 Kristo anafanana kabisa na Mungu asiyeonekana. Yeye ali kuwepo kabla Mungu hajaumba kitu cho chote. Yeye ndiye ali yeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake.

Msalaba

Wakolosai 1:19

1 Cor. 1:18 

Wafilipi 2:8 

Wakolosai 2:14

Waebrania 12:2

Wakolosai 1:19- Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamil ifu wake wote wa kimungu uwe ndani ya Mwanae;  

Udini

Mathayo 7:15

Mathayo 24:11

Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali.

Nguvu za giza

Matendo 26:17-18

Waefeso 5:8

Yohana 3:19 

Warumi 13:12

'Nitakuokoa kutoka kwa watu wako na watu wa mataifa. Ninakutuma ukawafungue macho yao ili watoke kwenye giza waingie nuruni na watoke katika nguvu za shetani wamgeukie Mungu; ili wapokee msamaha wa dhambi na wapate nafasi pamoja na wote ambao wanatakaswa kwa kuniamini.'

Mauti

Waebrania 9:27

Zaburi 116:15 

Ezekiel 33:11

Mhubiri  9:2-3

Na kama ambavyo mwanadamu ameandikiwa kufa mara moja tu, na baada ya hapo kukabili hukumu;t.  Zaburi 116:15 Ina thamani machoni pa BWANA mauti ya Wacha Mungu wake.

Maamuzi

Yakobo 1:5-8

Yoshua 24:15

 Lakini kama mtu ye yote kati yenu akipungukiwa na hekima, basi na amwombe Mungu, ambaye huwapa watu wote kwa ukarimu pasipo kulaumu, naye atapewa. 6Lakini aombe kwa imani pasipo shaka yo yote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari ambalo husu kumwa na upepo, likitupwa huku na huku. 7Mtu kama huyo asidhani atapata kitu cho chote kutoka kwa Bwana; 8kwa maana yeye ni mtu mwenye nia mbili asiyekuwa na msimamo katika jambo lo lote.

Mapepo

Waefeso 6:12

Luka 9:1

1 Timotheo 4:1

 Kwa maana hatupambani na bina damu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Huzuni/ Majonzi

Mithali 12:25

Zaburi 42:11

Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neon juma huufurahisha.

Zaburi 42:11 – Nafsi yangu ,kwanini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwamaana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, na Mungu wangu.

Mahitaji

Zaburi 37:4

Mithali 13:4 

Waefeso 2:3

Marko 4:19 

Wagalatia 5:24

Nawe utajifurahisha kwa BWANA, naye atakupa haja za moyo wako.

Mithali 13:4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa. Wagalatia 5:24Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na tamaa zake.

 

Uthabiti

Isaya 50:7

Mhubiri. 8:11

Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, name njua kuwa sitaona haya.

Ibada

1 Nyakati 28:9

Hesabu 14:24

Nawe, Suleiman mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, umtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo ya fikira; ukimtafuta ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.

Busara

Yakobo 1:5

Matendo 17:11

Lakini kama mtu ye yote kati yenu akipungukiwa na hekima, basi na amwombe Mungu, ambaye huwapa watu wote kwa ukarimu pasipo kulaumu, naye atapewa. Watu wa Beroya walikuwa waungwana zaidi kuliko watu wa Thesalonike. Walisikiliza neno la Mungu kwa hamu wakachambua Maandiko kila siku ili waone kama waliyokuwa wakiam biwa na Paulo ni kweli.

Uwanafunzi

Mathayo 28:19-20

2 Timotheo 2:1-2

Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu: mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Na kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.<

Utii

1 Wakorintho 9:26-27  Waebrania 12:5-8

Mithali 22:6,15, 23:13-14

Mimi sikimbii pasipo kuwa na lengo. Sipigani kama mtu anayepiga hewa; 27lakini nauimarisha mwili wangu na kuutawala, ili baada ya kuwahubiria wengine, mimi mwenyewe nisije nikakataliwa.

Ubaguzi

Wagalatia 3:28

Yakobo 2:1,9

Hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanaume na mwanamke. Wote mmekuwa kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu

Udanganyifu

Mithali 13:11

Mithali 12:22, 20:17

Mali ipatikanayo kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa. Mithali 20:17 -  Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu; Lakini halafu kinywa chake kitajaa changarawe.

Mafundisho

2 Timotheo 1:13-14,3:16 

Yohana 7:17

Waefeso 4:14 

1 Timotheo 4:16

Tumia kama kielelezo cha mafundisho sahihi maneno ya kweli ambayo umeyasikia kutoka kwangu pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu. Linda ile kweli ambayo umekabidhiwa na Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu. Andiko zima lina pumzi ya Mungu nalo lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki

Mashaka

Mathayo 21:21

Yakobo 1:5-6

Yesu akawajibu, ``Nawaambia kweli, kama mna imani na msiwe na mashaka hata kidogo, mtaweza kufanya yaliy ofanyika kwa huu mtini; na hata mkiuambia mlima huu, `Ng'oka, nenda kajitupe baharini,' itafanyika.

Ulevi

Waefeso 5:18

Mithali 20:1,23, 29-32

Pia msilewe divai, kwa sababu huo ni upotovu, bali mjazwe Roho. Mithali< 20:1 – Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosae kwa vitu hivyo hana hekima.

Dunia

Gen 1:1,10

Psalm 24:1

Mathayo 5:5 

Marko 13:31 

Yohana 3:31

Ufunuo 21:1

Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. Mwanzo 1:10  Mungu akapaita pale pakavu nchi; na makusanyiko ya maji akayaita bahari; Mungu akaona yakuwa ni vyema. Zaburi. 24:1  Zaburi ya Daudi. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.

Utu Wema

Waefeso 4:15-16

1 Wathesalonike 5:11

Badala yake, tukiambiana ukweli kwa upendo, tutakua kwa kila hali, tufanane na Kristo ambaye ndiye kichwa. Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeunganishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo vyake, hukua na kujengeka katika up endo, kila sehemu ikifanya kazi yake. Maisha Mapya Ndani Ya Kristo.

Elimu

Wafilipi 1:9-10

Zaburi 94:10

Mithali 1:7

Na sala yangu kwa ajili yenu ni kwamba upendo wenu uzidi kuongezeka siku hadi siku pamoja na maarifa na busara 10ili mpate kutambua mambo yaliyo mema. Na pia mpate kuwa watu safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo.

Fadhaa

Warumi  1:16

Yeremia 6:16

Mimi siionei aibu Injili kwa maanani nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia.

Maono ya Furaha au Huzuni

Mithali 4:23, 15:13

Mwanzo 30:2,13

Mwanzo 40:6

Linda moyo wako kuliko vyote ulindavyo; Maana ndiko zitokako chemchem za uzima. Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.

Ajira

Mhubiri 9:10

Waefeso 6:5-7

1 Wathesalonike 3:10-12

Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.Waefeso 6:5-6

Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo.

Kutia Moyo

1 Wathesalonike 5:14

Matendo 11:23,20:2  Wafilipi 2:19

Na tunawasihi, ndugu wapendwa, muwaonye wale walio wavivu, watieni moyo walio waoga, wasaidieni walio dhaifu na muwe na subira na kila mtu.

Wivu

Zaburi 37:1

Mithali 14:30, 23:17

Mathayo 27:17-18 Matendo 13:45

Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili.
Mithali. 14:30 Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.

Uzima wa Milele

Yohana 3:15

Tito 1:2

Yohana 5:24

1 Yohana 5:13

… ili kila mtu aniaminiye awe na uzima wa milele  Tito 1:2 ... na katika tumaini la uzima wa milele ambalo Mungu, ambaye hasemi uongo, aliahidi hata kabla dunia haijakuwepo.

Uinjilisti

Marko 16:15

Mathayo 18:18-20

Matendo 1:8

Akawaambia, ``Nendeni ulimwenguni kote, mkawahubirie watu wote Habari Njema.  

Uovu

Mwanzo. 3:5,6:5

Mathayo 12:35, 15:19

Yohana 3:19-20

Kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayo kula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.

Udhuru/ Kisingizio

Warumi 1:20

Luka 14:16-20

Yohana 15:22

Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio. .  Yohana 15:22 - Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia. Lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi zao.

Imani

Warumi 5:1,10:17

Waefeso 2:8-10

Waebrania 11:1,2,6

Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo. Warumi 10:17 Basi, chanzo cha imani ni kusikia, na kusikia huja kwa kuhubiri neno la Kristo.

Mastaka ya Uwongo

Isaiah 5:20

Mathayo 26:59-60

Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu! 

Walimu wa Uongo

Warumi 16:17-18

2 Petro 2:1-2

Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na wote wanaoleta mafara kano na vipingamizi kinyume cha mliyopokea. Waepukeni. 18Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno matamu ya kudanganya, hupo tosha mioyo ya watu wanyofu.

Familiya

Waefeso 2:19

Mwanzo 1:27-28

Kwa hiyo, ninyi sasa siyo wageni tena wala wapita njia, bali mmekuwa raia halisi pamoja na watu wa Mungu na familia ya Mungu.

Kufunga

Mathayo 6:16, 17:21

Marko 2:18

1 Wakorinto 7:5

Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao.

Hofu

Yoshua 1:9

Zaburi  27:1

Mathayo 10:28 

2 Timotheo 1:7 

Waefeso 5:21

Je! Si mimi niliye kuamuru?uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.Zaburi. 27:1 BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu nimhofu nani?

Ushirika

Yohana 13:34

1 Yohana 1:3

Nina waachia amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi. Kama mimi nilivy owapenda, na ninyi mpendane vivyo hivyo

Fedha/ Mapato

Malaki 3:10

Luka 6:38

1 Timotheo 6:6

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sita wafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni Baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha,au la.  Luka 6:38 - Muwe wepesi wa kutoa nanyi mtapokea. Kipimo mtakachotoa mtar udishiwa kikiwa kimejaa na kushindiliwa na kutikiswa na kufurika. Kwa kuwa jinsi mtakavyotoa, ndivyo mtakavyopata.''

Upumbavu

Mithali 24:9 

1 Wakorintho 1:18,21,25        Mithali  22:15

Fikira za mpumbavu ni dhambi, na mwenye mzaha huwachukiza watu. Mithali<. 22:15 -  Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; lakini fimbo ya adhabu itafukuzia mbali.

Msamaha

Isaya 1:18

Mathayo6:12-14,

21,22

Wakolosai. 3:12-13

Haya njooni tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Lugha Chafu

Waefeso. 4:29, 5:4

Mathayo 15:19 

Kutoka  20:7

Msiruhusu maneno machafu yatoke vinywani mwenu, bali mazungumzo yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika

Uhuru

Warumi 6:6-8,18

Yohana 3:34-36

Yohana 8:32,34

Tunafahamu kwamba mwili wetu wa asili ulisulubiwa msalabani pamoja na Kristo ili mwili wetu wa dhambi uharibiwe kabisa na tusiwe tena watumwa wa dhambi. Kwa maana mtu anapokufa anakuwa huru na mambo ya dhambi. Lakini ikiwa tumekufa na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. 

Urafiki

Mithali  17:17

Yohana 15:13-15

Mithali 18:24

 

Rafiki hupenda siku zote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.Yohana 15:13-15 Hakuna mtu mwenye upendo unaozidi ule wa mtu anayejitoa afe kwa ajili ya rafiki zake. 14Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafa nya ninayowaagiza. 15Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha.

Matunda

Mathayo 7:15-20

Warumi 7:4

Yohana 15:1-5 

…Mtawatambua kwa matunda yao<.  Philipian 1:11  Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa.

Wakati Ujao

Habakuki 2:3

Mathayo 6:34

Yakobo 4:13-14

Maana njozi hii ni kwa wakati ulio amriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapo kawia, uingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haita kawia.

Utoaji

Waebrania 13:16

Luka 6:38

Mathayo 10:8

Msiache kutenda mema na kushirikiana mlivyo navyo, kwa maana sadaka kama hizi ndizo zinazompendeza Mungu.  Luka 6:38- Muwe wepesi wa kutoa nanyi mtapokea. Kipimo mtakachotoa mtar udishiwa kikiwa kimejaa na kushindiliwa na kutikiswa na kufurika. Kwa kuwa jinsi mtakavyotoa, ndivyo mtakavyopata.''

Kutukuza

Isaya 25:1

Mathayo 5:6

Warumi 15:6 

1 Wakorintho. 6:20

Ee BWANA, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako.Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale kwa uaminifu wa kweli.

Ulafi

Wafilipi 3:19  Mithali 13:21 Luka 7:34

Mwisho wa watu hao ni kuangamia, na Mungu wao ni tumbo; kwa sababu wao huyaonea fahari mambo ya aibu na mawazo yao yametawaliwa na mambo ya dunia

Mungu

Mwanzo 1:1

Isaya 44:6,8

Kutoka 20:2,3

Yohana 1:1-2 

Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.Isaya. 45:14…watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana Mungu mwingine, hapana Mungu mwingine tena.

Mapenzi ya Mungu

Marko 3:35

1 Timotheo 2:4

2 Petro 3:9

Luka 7:30

Mtu ye yote anayetenda mapenzi ya Mungu ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.'' 

Matendo. 22:14-Akasema, `Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe ufahamu mapenzi yake…

Injili

Warumi 1:16-17 Marko 16:15

Luka 9:6

1 Wakorintho. 15:1-4

Mimi siionei aibu Injili kwa maanani nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia. Kwa maana Habari hii Njema inaonyesha wazi haki inayotoka kwa Mungu. Haki hii hupatikana kwa imani tangu mwanzo hadi mwisho. Kama ilivyoandikwa: ``Wenye haki wataishi kwa imani.''

Umbea

Mithali 16:28, 20:19,26:20

2 Wathesalonike 3:19

Mithali 16:28-Mtu mshupavu huondasha fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki. Mithali. 26:20 Moto hufa kwa kukosa kuni; Bila mchongezi fitina hukoma.

Serikali

Warumi 13:1

Isaya 9:6

Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.

Neema

Waefeso 1:7-8  Mwanzo 6:8

Waefeso 2:5-8

Warumi. 3:29,5:15,20

Tito 2:11

Kutoka kwake, tunapata ukombozi kwa ajili ya damu yake, yaani, kusamehewa dhambi zetu; kulingana na wingi wa neema yake 8ambayo ametumiminia kwa wingi  < Tito 2:11 Kwa maana neema ya Mungu iletayo wokovu imedhihirishwa kwa watu wote….

Uchoyo

Luka 11:39

1 Timotheo 1:3

 Ndipo Bwana akamwambia, ``Ninyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje huku ndani mmejaa udhalimu na uovu.

Huzuni

2 Wakorintho 1:3-4

Warumi 53:3 

Romans 9:1-3

Ashukuriwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja zote. Yeye anatufariji katika mateso yetu yote ili tuweze kuwafariji wale walio katika mateso yo yote, tukitumia faraja ambayo sisi tumepokea kutoka kwa Mungu . <

Kuongozwa

Mithali 3:5-6

Yeremia 10:23

2 Wathesalonike. 3:5

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, nae atayanyoosha mapito yako.

Hatia

Zaburi 32:5 

Ezra 9:13-15

Ezekiel 18:20

Yakobo 2:10

Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, nitayakiri maovu yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.

Yakobo. 2:10 - Kwa maana mtu ye yote anayetimiza sheria yote isipokuwa akashindwa kutimiza sehemu moja tu, amekuwa na hatia ya kuvunja sheria yote.

Machukio

Mithali 6:16-19

1 Yohana 4:20-21 Mathayo 5:43,44 Luke 6:27

Mtu akisema, ``Nampenda Mungu,'' na huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona.f someone says,” 1 Yohana 4:21 Na Mungu mwenyewe ametupa amri hii kwamba, mtu anayempenda Mungu hana budi kumpenda pia na ndugu yake. 

Moyo

Mathayo 22:37  Mithali 4:23

Yeremia 17:9

Mathayo 15:19

Warumi 10:8-10

Yesu akamjibu, ``Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.' Mithali. 4:23 Linda moyo wako kuliko vyote ulindavyo; Maana ndiko zitokako chem. Chem. Za uzima.  <

Mbinguni

Mathayo 7:21, 8:11,10:21

Luka 15:7,10:26

``Si kila mtu anayesema, `Bwana, Bwana,' ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Matendo 7:55 Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, akamwona Yesu amesimama upande wa kulia wa Mungu.''

Kuzimu

Zaburi  86:13

Luka 12:4-5

Luka 16:22-24

Ufunuo  20:15

Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu. Zaburi. 9:17 Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

Utakatifu

Warumi 12:1

Waebrania 12:14

1 Petro 1:15-16

Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu, jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu, ambayo ndio ibada yenu ya kiroho.

Roho Mtakatifu

Warumi 8:11

Yohana 14:16-17,25, 26,16:13-14

Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu.

Uaminifu

Waefeso 4:25

Walawi 19:36

Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja.

Tumaini

Warumi 15:13

Tito 3:7

Waebrania 6:18-19, 10:23

Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha na amani katika kumwamini, ili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mpate kuwa na tumaini tele. Tito 3:7- Na tukishahesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele tunaoutumainia . < <

Ukarimu

Warumi 12:13

1 Petro 4:9

3 Yohana 5,6

…Wasaidieni watu wa Mungu walio na shida. Muwe wakarimu kwa matendo.< 1 Petro. 4:9 Karibishaneni pasipo manung'uniko.

Unyenyekevu

Luka 14:11

Yakobo 4:10

"Kwa maana kila mtu anayejitukuza atash ushwa naye ajishushaye atatukuzwa.'' Jinyenye keshe mbele za BWANA , nae atakuinua. 

Unafiki

Luka 12:1-2 

Isaya 29:13

 Wakati huo, maelfu ya watu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu alizungumza na wanafunzi wake kwanza, akawaambia: ``Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao. ``Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana.

Bwana akanena, kwa kuwa watu hawa wananikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao imefarakana name, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa.

Ibada ya sanamu

Yoshua 24:14

1 Wakorintho. 10:4

Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo yam to, na huko Misri; Mkamtumikie yeye BWANA.

Ujinga

Waefeso 4:18

Matendo 17:30

1 Petro 2:15

Watu hao akili zao zimetiwa giza wasiweze kuelewa; nao wametengwa mbali na uhai wa Mungu kwa sababu ya ujinga walionao na ugumu wa mioyo yao.

Uovu

Waefeso 4:21-24

1 Wathesalonike. 4:3

1 Wakorintho 6:18,10:8

1 Wakorinto…Kimbieni dhambi ya zinaa. Dhambi nyingine zote anazotenda mwanadamu hufanyika nje ya mwili wake, lakini anayezini, ana tenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. . 1 Wathesalonike. 4:3 Mungu anapenda ninyi muwe watakatifu, mjiepushe na maisha ya zinaa;

Kuwa ndani ya Kristo

2 Wakorintho. 5:17

Wagalatia 6:15

2 Timotheo 1:9

1 Petro 5:14

Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, mapya yamekuja. . Wagalatia. 6:15 Kwa maana, kutahiriwa au kutota hiriwa si kitu kwangu; kitu cha maana ni maisha ya watu kubadili ika kuwa mapya.

Matukano

Luka 6:22

Luke 18:32

Waebrania 10:29

Mmebari kiwa ninyi watu watakapowachukia na kuwakataa na kuwatukana na kuharibu sifa yenu kwa ajili yangu.  Luka 18:32 Nitatiwa mikononi mwa watawala wa Kirumi. Watu watanizomea, watanitukana na kunitemea mate.

Ukamilifu

Mithali 10:9, 19:1,20:7

Tito 2:7

Aendaye kwa unyofu huenda salama; Bali apotoshaye njia zake atajulikana. Mithali. 19:1 Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa midomo alie mpumbavu.

Kitisho

Zaburi 46:1-3,

112:7-8

Waefeso 6:19-20

1 Thess. 2:4

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada unao onekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, ijapo pepesuka milima na kiburi chake. Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini BWANA. Moyo wake umethibitika hataogopa, hata awaone watesi wake wameshindwa. Waefeso. 6:19-20 Niombeeni mimi pia, ili kila ninapozungumza, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili pasipo woga. 20Mimi ni balozi kifun goni kwa ajili ya Injili hii. Kwa hiyo niombeeni niihubiri Injili kwa ujasiri kama inipasavyo.  1 Wathesalonike. 2:4 -Kinyume chake, tunahubiri kama watu tuliopata kibali cha Mungu tukakabidhiwa Habari Njema. Nia yetu si kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu anayejua mawazo ya mioyo yetu. 

Wivu

Kutoka  34:14

Hesabu 5:12-28

Yakobo 4:4-5

Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.

Yesu Kristo

Matendo 2:38

Mathayo 1:1-12, 18-24

Matendo 2:38 Petro aliwajibu, ``Tubuni, muache dhambi na kila mmoja wenu abatizwe katika jina la Yesu Kristo, ili msamehewe dhambi zenu; nanyi mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu.

Furaha

Zaburi 30:5,32:11

Luka 15:10

1 Yohana 1:4

1 Petro 1:8

Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake kuna uhai.  1 Yohana 1:4 -  Tunawaandikieni mambo haya ili furaha yetu ikamilike.

Hukumu

Zaburi 9:7-8

Matendo 17:30

2 Wakorintho. 5:10

Ufunuo. 20:11-13

Bali BWANA atakaa milele, Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu. Naye atahukumu ulimwengu kwa haki; atawaamua watu kwa adili.  

Haki

Kumb. 10:17-18

Luka 11:42

Kwa maana BWANA mungu wenu, yeye ndie Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa. Kumb. 10:18 Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, nae humpenda mgeni akimpa chakula na mavazi.

Wema/ Fadhili

Zaburi 117:2 

Tito 3:4-5 

2 Petro 1:5-8

Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na uaminifu wa BWANA ni wa milele.

Ufalme wa Mungu

Yohana 3:3 

Matendo 19:8

Warumi 14:17 

1 Wakorintho 6:9-10

Luka 18:16

Yesu akamjibu, ``Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.''

Elimu/ Maarifa

1 Samueli 2:3 

Zaburi 119:66 

Mithali 1:7,22

Msizidi sana kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa, na matedo hupimwa nay eye kwa mizani.

Uvivu/ Uzembe

Mhubiri. 10:18

Mithali 13:4, 19:24,20:4

Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa utepevu wa mikono nyumba huvuja.

Uongozi

Luka 6:39

Mathayo 6:13

Waebrania 13:7-17

Pia akawapa mfano akasema, ``Je, kipofu anaweza kumwon goza kipofu mwenzake? Si wote wawili watatumbukia shimoni?  Matayo. 6:13 – Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,' [Kwa kuwa Ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele. Amina.]

Uhai

Yakobo 4:14

Yohana 14:6

Kumbe hamjui litakalotokea kesho! Kwani maisha yenu ni kitu gani? Ninyi ni kama ukungu ambao huonekana kwa muda mfupi tu na baadaye hutoweka.

Nuru

Yohana 8:12 

Mwanzo 1:3

Zaburi 44:3, 119:105

Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, ``Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru yenye kuleta uzima.''

Upweke

Mwanzo 2:18,21-25

Marko 15:34

Mhubiri. 4:9-10

BWANA Mungu akasema, si vyema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae.

Meza ya Bwana

1 Wakorintho. 11:20,

23-29

Luka 22:7-20

021Kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu…

Upendo

Yohana 3:16

1 Yohana 3:14

1 Yohana 4:7,16

Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu.

Uaminifu

1 Yohana 3:16

Yohana 15:13

Hesabu 12:7

 Na tumeujua upendo kwa sababu Kristo alitoa maisha yake kwa ajili yetu. Na sisi tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu.

Tamaa Mbaya

Wagalatia 5:16 

1 Yohana 2:16 

Yakobo 1:13-15

Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili.  1 Yohana 2:16 Maana vitu vyote vil ivyomo duniani, yaani, tamaa za mwili, tamaa ya vitu vinavyoone kana kwa macho, na kiburi kiletwacho na mali, vyote hivi havitoki kwa Baba bali hutoka ulimwenguni.

Uongo

Mithali  6:16-19, 12:22,13:5,

Waefeso 4:25

Kuna vitu sita anavyo vichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Mithali 6:17-19 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia. Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Ndoa

Waebrania 13:4

Mwanzo 2:21-25

Ndoa iheshimiwe na watu wote, na wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati.

Upole

Hesabu 12:3

Zaburi 37:11

Wakolosai 3:12

Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.  Zaburi 37:11- Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.

Rehema

Hesabu 14:18 Zaburi 25:10  Mathayo 5:7

Yakobo 5:11

BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yoyote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne.

Akili/ Dhamira

Isaya 26:3

Mathayo 22:37 

1 Wakorintho 1:10

Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

Umisheni

Mathayo 28:18-20

Matendo 1:8

Warumi 10:13-15

Matayo 28:18-20  Yesu akawakaribia akawaambia, ``Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu: mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Na kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Pesa

1 Timotheo 6:10  Mithali 11:28 

Luka 18:24

1 Timotheo 6:17

Maana kupenda fedha ni chanzo cha uovu wote. Tamaa ya fedha imewafanya wengine watangetange mbali na imani na kuteseka kwa huzuni nyingi.

Mziki

Mwanzo 4:21

1 Nyakati 13:8 

Zaburi 33:2 

Waefeso 5:19

Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo niye baba yao wapigao kinubi na filimbi. Zaburi.33:2 – Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.

Jirani

Luka 10:27-37

Mithali 37:10  Warumi 13:10

Yule mwalimu wa sheria akajibu, ``Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote. Na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwe nyewe.'

Utii

1 Samueli 15:22  Matendo 5:29 

Waefeso 6:1 

2 Wathesalonike 1:8

Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na zabihu sawasawa na kutii sauti ya BWANA? Angalia kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Ummoja

Yohana 10:30 

Yohana 17:11  Matendo1:14

Mwanzo 2:24 

Mathayo 19:5

Mimi na Baba yangu tu mmoja.''Yohana 17:11- Mimi naondoka ulimwenguni ninakuja kwako. Lakini wao wako ulimwenguni. Baba Mtakatifu, walinde kwa jina lako ambalo umenipa ili wawe na umoja kama sisi tulivyo mmoja.

Yatima

Yakobo 1:27 

Yohana 14:18

Dini iliyo safi, isiyo na uchafu mbele za Mungu Baba, ndio hii: kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu.

Maumivu

Mwanzo 3:16 

Ufunuo 16:10 

Ufunuo 21:4

Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa mtoto; na tama yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.

Wazazi

Kumb. 6:6-7 

Waefeso 6:1

2 Wakorintho 12:14

Waebrania 11:23

Na maneno haya ninayo kuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; Kumb. 6:7 Nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo na uondokapo.

Adhabu

Kumb. 1:17

Matendo 10:34  

Warumi 2:11

Yakobo 2:1,9

Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neon liwashindalo mniletee mimi, name nitasikiliza.

Uvumilivu

Nehemia 9:30

1 Timoteo 6:11  Yakobo 1:3,5:10

Luka 21:19

Lakini miaka mingi ukichukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako kwa vinywa vya manabii wako; wao wasitake kusikiliza; kwahiyo ukawatia katika mikono ya watu wan chi. Luka 21:19 - Simameni imara nanyi mtaokoa nafsi zenu.''

Amani

Hesabu 6:26 

Psalm 37:11

Mithali 16:7

Isaya 26:3

Wafilipi 4:6

BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani. Wafilipi 4:6 -  Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru.

Ukamilifu

Waebrania 6:1 

wakolosai 3:14

Basi sasa tutoke katika yale mafundisho ya msingi kuhusu Kristo, tupige hatua kufikia ukamilifu katika kuelewa kwetu. Hatupaswi tena kuwaeleza ninyi yale mafundisho ya msingi kuhusu kutubu na kuacha matendo yaletayo kifo, na kuhusu kumwamini Mungu

Udhalimu/ Mateso

2 Timotheo 3:12 Mathayo 5:11  John 15:20 Warumi 12:14

Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya kumcha Mungu ndani ya Kristo Yesu watateswa. Warumi 12:14 - Waombeeni baraka za Mungu wanaowatesa. Wabarikini wala msiwalaani.

Uvumilivu

Warumi 5:3-4

Waefeso 6:18 

Yakobo 5:11

Kwa kupitia kwake tumepata njia ya kufikia neema hii ambayo inatuwezesha kusimama imara, tukifurahia tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu. Warumi 5:4 na subira huleta uthabiti wa moyo; na uthabiti wa moyo hujenga tumaini.

Maskini

Kumb. 15:11

Ayubu 36:15 

Mithali 17:5

Luka 6:20

Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo nitakapo kuamuru na kukwambia, Mfumbulie kwakweli mkono wako nuguyo, mhitaji wako, masikini wako, katika nchi yako.

Nguvu

Zaburi 62:11

Yeremia 51:15

Marko 13:26 

Warumi 1:16

2 Samweli 22:33

Maramoja amenena Mungu; Mara mbili nime yasikia haya, Ya kuwa nguvu zi na Mungu.Yeremia. 51:15 -  Ameumba dunia kwa uweza wake… 2 Samweli. 22:33 – Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia zake.

Sifa

Zaburi 30:4, 35:8, 69:34 

Waebrania 13:15

Waefeso 1:12

Mwimbieni BWANA zaburi, enyi watumwa wake. Na kufanya shukurani kwa kumbukumbu la utakatifu wake. Waefeso 1:12 - Kwa njia hiyo, sisi ambao tulikuwa wa kwanza kumtegemea Kristo, tupate kuishi maisha yatakayoleta sifa kwa utukufu wake

Maombi

Mithali 15:8,29  Mathayo 7:7 

Wafilipi 4:6  James 5:16

The sacrifice of the wicked [is] an abomination to the LORD, But the prayer of the upright [is] His delight. Pro.15:29 The LORD [is] far from the wicked, But He hears the prayer of the righteous.

Kuwaombea Wapendwa katika Kristo (1)

Waefeso 1:16-20,

3:14-21,6:18

 

sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, na kuwakumbuka katika sala zangu. Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni roho ya hekima na ya mafunuo mpate kumfahamu zaidi. Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu; na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni. Kwa sababu hii napiga magoti mbele ya Mungu Baba, aliye baba wa familia ya waamini wote, mbinguni na duniani. Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyoni mwenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake. Na naomba kwamba, kwa imani, Kristo aendelee kuishi ndani ya mioyo yenu, ili mkiwa mmesimama imara na kujengwa katika upendo, mpate uwezo wa kuelewa, pamoja na watu wote wa Mungu, upana na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo; na mpate kufa hamu upendo huu, ingawa unapita upeo wa maarifa, na hivyo mpate kujazwa kabisa na ukamilifu wa Mungu mwenyewe. Utukufu ni wake yeye, ambaye ana uwezo wa kutenda zaidi ya yale tunayoyaomba na kuyawazia, kwa kadiri ya nguvu yake inayofanya kazi ndani yetu. Utukufu ni wake katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amina. … Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu.

Kuwaombea Wapendwa katika Kristo  (2)

Wafilipi 1:3-11, 2:13,4:4-9

 

Ninamshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka katika sala zangu zote, nikiomba kwa furaha na shukrani kwa ajili ya ushi rikiano uliopo kati yetu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. Nina hakika kwamba, yeye aliyeianza kazi yake njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha siku ile ataka porudi Yesu Kristo.

 Ninajisikia hivi kwa sababu nawathamini sana moyoni mwangu. Kwa maana tumeshiriki pamoja neema ya Mungu wakati nikiwa kifun goni na wakati nikiitetea na kuithibitisha Injili. Mungu ni shahidi wangu kwamba natamani mno kuwa pamoja nanyi na kwamba upendo nilio nao kwenu ni upendo wa Kristo Yesu. Na sala yangu kwa ajili yenu ni kwamba upendo wenu uzidi kuongezeka siku hadi siku pamoja na maarifa na busara ili mpate kutambua mambo yaliyo mema. Na pia mpate kuwa watu safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo. 11Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa.

Kwa maana ni Mungu ambaye anatenda kazi ndani yenu, akiwapa nia ya kutimiza mapenzi yake na kuwawezesha kutenda yale yanayompendeza…. Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! Upole wenu ufahamike kwa watu wote. Bwana anakaribia kuja. Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu.

 Hatimaye ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo na sifa, yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo uzuri wo wote, pakiwepo na cho chote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. Mambo yote mliyojifunza au kupokea au kusikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatekelezeni. Na Mungu wa amani ata kuwa pamoja nanyi

 

Kuombea Wapendwa katika Kristo (3)

2 Wathesalonike 1:11-12,2:13-17,

3:1-5,16

Kwa sababu hii tunawaombeeni bila kukoma, kwamba Mungu awahesabu kuwa mnastahili maisha aliyowaitia na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila nia njema mliyo nayo na kila tendo linalotokana na imani yenu. Tunaomba hivi ili jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwa ajili yenu nanyi mtukuzwe kwa ajili yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo…. Ndugu wapendwa, ninyi msi choke kutenda mema. Ikiwa mtu atakataa kutii maagizo tunayotoa katika barua hii, mwangalieni vema mtu huyo, mjitenge naye, ili apate kuona aibu. Lakini msimhesabu kama adui bali mkanyeni kama ndugu. Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa njia zote. Bwana na awe nanyi nyote. Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwe nyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Ndugu wapendwa, ninyi msi choke kutenda mema. Ikiwa mtu atakataa kutii maagizo tunayotoa katika barua hii, mwangalieni vema mtu huyo, mjitenge naye, ili apate kuona aibu. Lakini msimhesabu kama adui bali mkanyeni kama ndugu. Salamu Za Mwisho. Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa njia zote. Bwana na awe nanyi nyote. Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwe nyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa njia zote. Bwana na awe nanyi nyote.

Majivuno/ Kiburi

Mithali 13:10, 16:18

1 Yohana 2:16

Yakobo 4:6

Mithali 29:23

Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale

mso-bidi-font-family:"Times New Roman"; color:blackwanaozingatia shauri.  Mithali Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno kabla ya anguko. Mithali. Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.

 

Kipau Mbele

Mathayo 6:33

Mithali 3:9

Wakolosai 1:28 

1 Timotheo 4:8

Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa.

Kuchelewa

Matendo 24:25 

Kutoka 8:9-10  Mithali 3:27-28

Na Paulo alipokuwa akiwaeleza juu ya kuwa na kiasi na juu ya hukumu ya mwisho, Feliksi aliin giwa na hofu akasema, ``Tafadhali sasa nenda, nitakuita tena nikipata nafasi.''

Ahadi

2 Petro 1:4 

1Yohana 2:25  

Kumb. 15:6

1 Wafalme 8:56

Kwa njia hiyo ametupatia ahadi zake kuu na za tha mani. Mkishika ahadi hizo mtashiriki asili yake ya kimungu na kuepuka uovu ambao uko duniani kwa sababu ya tamaa mbaya.

Unabii

2 Petro 1:20-21

Ufunuo 22:18 

1 Petro 1:10

Kwanza kabisa ni lazima muelewe kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliotokana na tafsiri ya nabii mwenyewe.

2 Petro 1:21 - Kwa sababu hakuna unabii uliokuja kwa matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe kutoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Usafi

1 Timotheo 4:12, 5:22 

Mithali 12:6 

Zaburi 19:8

Mithali 20:11 Mathayo 5:8

Mtu asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe mfano mwema kwa waamini wote kwa maneno yako, kwa mwenendo wako, katika upendo, imani na usafi.  1 Timoteo. 5:22 - Usiwe na haraka kumwekea mtu mikono wala usishiriki katika dhambi za mtu mwingine, jiweke katika hali ya usafi.

Maswali

Luka 2:46 

1 Wakor. 10:27

 Siku ya tatu wakamkuta Hek aluni ameketi kati ya walimu wa sheria, akiwasikiliza na kuwau liza maswali.

Uasi

1 Samweli15:23

Waebrania 3:8

Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.  Kwa sababu umelikataa neno la BWANA, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.”

Wongofu

Tito 3:5

Mathayo 19:28

ali tuokoa, si kwa sababu ya matendo mema ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya huruma yake. Alituokoa kwa kuoshwa na kuzaliwa mara ya pili na kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu,

Marafiki

Mithali 12:26

Mithali 18:24

Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki, bali njia ya waovu huwapotosha.

 

Toba

Marko 1:4 

Mathayo 9:13  Acts 20:21

Luka 13:3

Yohana alitokea nyikani, akawabatiza watu huko na kuwahubi ria kwamba watubu, wabatizwe, ili wasamehewe dhambi zao. Luka 13:3 - Sivyo hata kidogo. Ninyi pia msipoacha dhambi zenu mtaangamia vivyo hivyo

Sifa Njema/mbaya

Mithali 25:10 Matendo 6:3 

Wafilipi 2:7

ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka.

Wafilipil 2:7 Bali alikubali kuacha vyote, akachukua hali ya mtumishi, akazaliwa na umbo la wanadamu.

Heshima

Zaburi 40:4

Isaya 17:7

Mathayo 21:37 Waebrania 12:9

Heri mtu yule amfanyae BWANA kuwa tumaini lake, wasiowategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.  Isaya 17:7 7Katika siku ile watu watamwangalia Mwumba  wao na kuelekeza macho yao kwa huyo Aliye Mtakatifu wa Israeli.

 

Majukumu

1 Nyakati. 9:27 

Ezekiel 10:4  

Warumi 15:27

Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi.

 

Pumziko

Mwanzo 2:1-2 

Kutoka 33:14

Kutoka 35:2

Matayo 11:28-29

Ufunuo 14:11,13

 

Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Mwanzo 2:2 Na siku ya saba Mungu akamaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. .

 

Ufufuo

Mathayo 28:1-6 

1 Wakorintho. 15:21 

Matendo 17:18

1 Petro 1:3

Hayupo hapa. Amefu fuka kama alivyosema. Njooni muone pale alipokuwa amelazwa.

1 Wakorintho. 15:21 -  Kwa maana kama vile kifo kilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja.

Lipiza (kisasi)

Warumi 12:19

Luka 6:27-28

Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:``Kisasi ni juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana.

Thawabu

Mathayo 16:27 Marko 9:41 

1 Wakor. 3:11-14

Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja katika utukufu wa Baba yangu pamoja na malaika wangu na nitamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Utajiri

1 Timotheo 6:7–9

Mithali 11:28

Mithali 22:1

Marko 10:24-25

Kwa maana hatukuja na kitu cho chote hapa duniani, wala hatuwezi kutoka na kitu. Mithali. 22:1 – Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.

Uadilifu

Mwanzo 15:6 

Zaburi 11:7

Zaburi 23:3 

2 Wakor. 5:21

Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.Zaburi 11:7  Kwa kuwa BWANA ndiye mwenye haki, Apenenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watamwona uso wake.

Sabato

Kutoka 16:26, 20:8

Mathayo 12:8,  12:12

Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni sabato, siku hiyo hakitapatikana.Kutoka 20:8-Ikumbuke siku ya sabato uitakase.

Huzuni

Nehemia 2:2, 8:9, 10

Mhubiri  7:3 

Yohana 16:20

Ufunuo 21:4

Basi mfalme akaniambia, mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, ispokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana. Ufunuo 21:4   Atafuta machozi yao yote, na kifo hakitakuwepo tena, wala maom bolezo, wala kilio, wala maumivu; maana mambo hayo yote ya awali yamekwisha toweka.''

Wokovu

1 Nyakati 16:23

Zaburi 3:8

Matendo 4:12

Warumi 1:16

2 Wakor. 6:2 

Waebrania 2:3

Mwimbieni, BWANA nchi yote; tangazeni wokovu wake siku kwa siku. Zaburi 3:8 – Wokovu u na BWANA: Baraka yako na iwe juu ya watu wako. Heb. 2:3 -sisi je? Tutaepukaje kama tusipojali wokovu mkuu namna hii?...

Utakatifu

1 Wathes. 4:3 

2 Wathes. 2:13

1 Wakor. 6:11

Waebrania 10:10

Mungu anapenda ninyi muwe watakatifu, mjiepushe na maisha ya zinaa; Waebrania 10:10 Na kwa mapenzi hayo, sisi tumetakaswa kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu, kwa wakati wote.

Shetani

Mwanzo 3:3-5 

Job 1:6

Mark 1:13 

Rev. 20:10

Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu, Ayubu 1:6 Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, shetani nae akaenda kati yao.

Kuja kwa mara ya pili

Ufunuo 1:7 

Zekaria 14:1

Mathayo 24:27-42  Yohana 14:1-3 

Hebrews 10:37

Tazama! Anakuja katika mawingu! Na kila jicho litamwona. Hata na wale waliomchoma mkuki na makabila yote ulimwenguni wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.

Ubinafsi

2 Timotheo 3:2 

Wafilipi 2:3 

Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio na utakatifu;

Kiburi/ Kujiona bora

Waebrania 10:35 

Wakolosai 1:21-22,2:10

Kwa hiyo msitupe tumaini lenu, ambalo litapewa tuzo kubwa. Wakolosai 2:10 - anyi mmepewa ukamilifu ndani ya Kristo, ambaye yeye ni mkuu juu ya kila uwezo na kila mamlaka.

Utumishi

Mathayo 20:26  Marko 9:35 

Luka 16:13

Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, anayetaka kuwa mkuu kati yenu hana budi kuwa mtumishi wenu.

Magonjwa

Mithali 18:14  Mathayo 4:23 

2 Timotheo 4:20

Yakobo 5:14

Marko 2:17

Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake; Bali roho iliyo vunjika ni nani  awezaye kuistahimili?

Marko 2:17 -   Yesu aliposikia haya aka waambia, ``Wenye afya nzuri hawahitaji daktari, bali wagonjwa wanamhitaji. Sikuja kuwaalika wenye haki, bali wenye dhambi.''

Dhambi

Warumi 6:23, 5:8,5:12

1 Yohana 1:8-9

Zaburi 119:11 

Mithali 20:9

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Zaburi 119:11 -  Moyoni mwangu nimeweka neon lako, nisije nikatenda dhambi. Mithali 20:9 -  Nani awezaye kusema, nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu?

Umoja

2 Nyakati. 30:12

Matendo 2:46 

Sefania 3:9

Tena katika Yuda mkono wa Mungu ulikuwa ukiwapa moyo mmoja, waitimize amri ya mfalme na wakuu kwa nena la BWANA.

Huzuni

Mithali 23:29 Mithali 10:22  Nehemia 8:10

Mwanzo 3:16

Ni nani apigaye, yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?Ni nani aliye na jiraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?

Nafsi

Mwanzo 35:18

Walawi 17:11

Mathayo 10:28,

16:26

Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini. Mathayo 16:26 - ``Kwa maana mtu atapata faida gani akiupata ulimwengu wote lakini akaipoteza nafsi yake? Au mtu atabadilisha nini na nafsi yake?

Maneno/ Mazungumzo

Zaburi 19:2:3 

Mwanzo 11:1 

Mithali 17:7

Wakolosai 4:6

Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. Zaburi 19:3  Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Kolosai  4:6 - Mazungumzo yenu yawe ya unyen yekevu wakati wote, yawe ya kuvutia, ili mjue jinsi ya kumjibu kila mtu.

Karama za Roho

1 Wakor.12:1,4 -11

Waefeso 4:7-8

Sasa kuhusu karama za Roho Mtakatifu ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu. Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni mmoja.

Shida/ Msongo

Zaburi 143:4 

Mathayo 26:37

Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka.

Ukaidi

1 Samueli15:23  Mithali 29:1

Zaburi 81:12

Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umulikataa neon la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme. Zab. 81:12 – Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao.

Utii

1 Petro 5:5 

1 Timotheo 2:11, 3:4 

1 Petro 3:1

Yakobo 4:7

Kadhalika ninyi vijana watiini wazee. Jivikeni unyenyekevu, mnyenyekeane kwa maana, ``Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu.''

Kujiua

1 Samueli  31:4  Mathayo 27:5

2 Samueli 17:23

Ndipo Sauli akamwambia Yule mchukuwa silaha zake, futa upanga wako unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa kunichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukuwa silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.

Mateso

Waebrania 2:9 

Yakobo 5:10,13  Yuda 1:7

Lakini tunamwona Yesu, ambaye kwa muda mfupi alifanywa kuwa chini kidogo ya mal aika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu aliteseka na kufa, ili kwa neema ya Mungu, aonje mauti kwa ajili ya watu wote.

Kufundisha

Mathayo 4:23, 7:28

Matendo 5:42 

Wakolosai 3:16

Yesu alizunguka Galilaya yote, akifundisha katika masi nagogi na kuhubiri Habari Njema ya Ufalme wa mbinguni, na kupo nya kila ugonjwa na kila udhaifu.

Majaribu

Mathayo 6:13, 26:41

Luka 4:13

1 Wakor. 10:13  Yakobo 1:12-15

Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,' [Kwa kuwa Ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele. Amina.].   Yakobo 1:14 - Lakini kila mtu hujaribiwa anapovutwa na kudanganywa na tamaa yake mwenyewe.

Ushuhuda

Kumb. 17:6 

Luka 9:5 

Matendo 22:12

2 Timotheo 1:8

Huyo atakaye uawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja.

Shukurani

Zab. 100:4

Warumi 1:21 

Wakolosai 3:15  

2 Timotheo 3:2

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Wakolosai  3:15 -  Ruhusuni amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena muwe na shukrani.

Majaribu

Luka 22:28

Matendo 20:19 

Yakobo 1:2

1 Petro 1:6

 ``Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu:Matendo 20:19 Nilimtumikia Bwana kwa unyenyekevu na machozi na kwa mateso yaliyotokana na njama za Wayahudi.

Maudhi/ Taabisha

Ayubu 14:1 

Zaburi 34:17

Mithali 21:23

Isaya 65:16 

Marko 3:18

"Mwanadamu aliye zaliwa na mwanmke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Zaburi 34:17 - [Walilia, naye BWANA akawasikia, akawaponya na taabu zao zote.

Tumaini

2 Samueli 22:31  Ayubu 13:15 

Zab. 2:12, 34:22, 37:5

1 Timotheo 4:10

Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya BWANA imehakikishwa; Yeye niye ngao yao wote wanaomkimbilia. 1 Tim 4:10 na kwa ajili yake sisi tunajitahidi na kutaabika, kwamba tumeweka tumaini letu kwa Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, hasa wale waaminio.

Kweli/ Hakika

Zab. 119:160

Yohana 14:6

Waefeso 1:13

1 Timotheo 2:4 

2 Timotheo 2:15 Waebrania 10:26

Jumla ya neno lako kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele. Yohana 14:6 Yesu akawaam bia, ``Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.

Kutoamini

Mathayo 13:58  Marko16:14 

Warumi 3:3

Waebrania 3:12, 19

Na hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.  Waebrania 3:12- Angalieni, ndugu zangu, asiwepo miongoni mwenu mtu ye yote mwenye moyo wa dhambi, usioamini, unaomfanya ajitenge na Mungu wa uzima.

Wasioamini

Luka 12:46

2 Wakor. 6:14

bwana wake atarudi siku ambayo hakumtazamia, na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamwadhibu vikali pamoja na wote wasiotii.

Umoja

Zaburi 133:1

Waefeso 4:3,13  Warumi 6:5

Tazama jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja na kwa umoja. Warumi 6:5 - Kwa maana ikiwa tumeunganika naye katika kifo chake, basi tutaunganika naye katika kufufuka kwake.

Kulipiza Kisasi

Warumi 12:19

Luka 6:27-28

Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:``Kisasi ni juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana.

Vita/ Ugomvi

2 Wakor. 10:4

1 Timotheo 1:18

2 Timotheo 2:4

Silaha zetu si za kidunia, bali silaha zetu zina nguvu ya kimungu iwezayo kubomoa ngome.  2 Timotheo 2:4 - Hakuna askari ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kiraia kwa sababu nia yake ni kumrid hisha yule aliyemwandika kuwa askari.

 

Angalia/ Chunga

1 Petro 5:8

2 Timotheo 4:5

1 Petro 4:7

Kaeni macho. Kesheni, maana adui yenu Ibilisi, huzunguka- zunguka akinguruma kama simba, akitafuta mtu atakayemmeza 1 Pet. 4:7 - Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo muwe na akili timamu na wenye kiasi ili mweze kuomba.  

Kuchoka/ Taabu

Wagalatia 6:9 

2 Wakor. 11:7 

Waebrania 12:3

Basi, tusi choke kutenda mema, kwa sababu kama hatukuchoka tutavuna kwa wakati wake.

Waovu

Zaburi 9:17 

Mithali 11:7

Yeremia 17:9 

Waefeso 6:16

Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanao msahau Mungu.

Zaburi 7:11 – Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhabikaye kila siku.

Busara

Zaburi 111:10

Mithali 3:19  Warumi 11:33

1 Wakor. 3:19 

Yakobo 1:5

Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele. Kwa hekima BWANA aliweka misingi ya nchi; Kwa akili zake alifanya mbingu imara;

Shahidi/ Ushuhuda

Matendo 26:22 

Matendo 22:15 

Matendo 1:8

Lakini mpaka wakati huu nimepata msaada uto kao kwa Mungu, na kwa hiyo nasimama hapa nikitoa ushuhuda wangu kwa watu wote, wakubwa kwa wadogo. Nami sisemi lo lote ila yale ambayo Musa na manabii walitabiri yangetokea:

Neno

Mathayo 4:4 

Yohana 1:1,14

Yohana 5:24

Matendo 8:4

Lakini Yesu akamjibu, ``Imeandikwa, `Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno analotamka Mungu.' '' Matendo 8:4 - Wale waamini waliotawanyika walihubiri neno la Mungu kila mahali walipokuwa.

Kazi

Mwanzo 2:2 

1 Wakor. 15:58 

2 Wathes.3:10-12

Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yotealiyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

Ulimwengu

Zaburi  89:11,96:13

Mathayo 5:4 

Marko16:5

Yohana 1:10

1 Yohana 2:15

Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyoNdiwe uliye upiga msingi wake.Yohana 1:10 - Neno alikuwepo ulimwenguni, lakini japokuwa aliumba ulimwengu, watu wa ulimwengu hawakumtambua!

Hofu

Mathayo 6:25,34 Mathayo 10:19

Luka 12:26

Wafilipi 4:6

``Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi?

Ibada

Kutoka 34:14

Zaburi 29:2

Mathayo 4:10

Yohana 4:24

Kwa maana huta mwabudu mungu mwingine,kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu, Mathayo. 4:10 -  Yesu akamwambia, ``Ondoka hapa shetani! Kwa maana imean dikwa, `Utamwabudu Bwana Mungu wako na utamtumikia yeye peke yake

Ghadhabu

Yohana 3:36 

Warumi 1:18,5:9  Waefeso 4:31,5:6

6Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake daima.''

Ujana

Zaburi  25:7  Mhubiri 12:1

1 Timotheo 4:12

Usikumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhilizako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.

Kujitoa/ Moyo

Tito 2:14

Romans 10:2

Tito. 2:14 -  Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe katika uasi wote, na kutufanya tuwe safi kwa ajili yake; na tuwe watu wake kabisa, ambao wana juhudi katika kutenda mema. Warumi 10:2 Ninashuhudia wazi kwamba wao wanajuhudi kubwa ya kumtumikia Mungu, lakini juhudi yao haitokani na kuelewa.