Maombi ya Mahitaji kwa Kiswahili - Imetolewa: 10/05/09

NCHI TAREHE-# MAHITAJI MAJIBU
Brazili 031509-1 Omba kwa ajili ya huduma ya  Mary & Martha waliopo Amazon River Basin wakiwahudumia wanawake wanao nyanyaswa na wenye kujihusisha na ukahaba. Wanaomba kupata mahitaji yao ya kila mwezi. Ombea kwamba Mungu anyanyuwe watu watakaoweza kuwapatia msaada wa  $1000 kwa kila  mwezi. 080309-Ruth ambaye ni mhusika wa hii huduma amesema wanauwezo wa kuendelea na huduma, lakini hawataweza kuikuza huduma hii bila msaada zaidi. Wafadhili wao wamewaongezea $100 nyingine.
 Brazili 100109-1 Kutokana na walivyoonekana kutoka katika ndege, wanakijij ambao hawajawahi kufikishiwa injili walionekana katika matawi yam to Amazon. Amepatikana mmishenari wa kwenda katika eneo hilo. Omba kwa ajili ya mahitaji na ulinzi wake. Jina lake ni Ndugu.  Albertin.  
 Brazili 100509-1 Mradi wa Amazon unahitaji boti ya aluminum pamoja na injini ya rabeta (long shaft) kwa ajili ya kutembea katika maji mtepesi kwa ajili ya wapanda makanisa kuweza kufikia maeneo 10 ya kupanda makanisa. Gharama ni $4000.  
 Cambodia 050509-1 Bruce na Margaret McKee wanaomba upenyo wa kufikisha huduma  yao ya wakambodia katika makanisa wakati wakiwa katika mapumziko yao nchini Marekani, maeneo ya Dallas Texas.  
 Cambodia 051309-1 Mchungaji Phen ameachwa na mke wake pamoja na mtoto wao . Anaomba Mungu amwonyeshe mpango mwema juu yake na mtoto wake.  
 Cambodia 100509-1 Mchungaji  Pich anahitaji  dola.500 kwa ajili ya watoto wasiojiweza wanaowatunza zisaidie ada na nguo za shule.  
 Cambodia 100509-2 Mchungaji  Pich na washirika wake wamenunuwa eneo miaka miwili iliyopita na wanahitaji dola 2532 za ujenzi wa jingo la kanisa katika jimbo la Kamport.  
 Cambodia 100509-3 Mchungaji Pich anaomba mfadhili wa kulisha watoto katika jumuiya yake mara moja kwa siku, na pia kulisha watoto wanaokuja kanisani jumapili. Kiwango chochote cha fedha kinahitajika.  
 Cambodia 100509-4 Mchungaji  Matthew amekuwa akipanga nyumba isiyokuwa na mabati, na sas ni wakati wa mvuwa. Anaweza akaezeka mabati kwa dola 200. Na itatumika kwa ajili ya darasa la kiingereza na kwa ajili ya kujifunza Bibilia.  
 Cambodia 100509-5 Mchungaji  Matthew anahitaji bibilia 30 kwa ajili ya wale wasioweza kununua  Biblia. Gharama ni dola 3.50 kila moja, na jumla ni dola 105.  
 China 033109-1 Omba kwa ajili ya  Roger and Hilde walioko China na wanategemea kumaliza masomo yao na kuendesha huduma ya kikristo kwa njia ya redio. Utamaduni wa kichina unategemea mtoto atunze wazazi wake wakati wa uzeeni, Wazazi wasio wakristo wana wasiwasi na maamuzi ya Rogers kuwa mmisionari kwamba ataaribu mategemeo yao ya baadaye. Tunaweza kupiga simu hii “tukajibiwa tumepata” Mambo yote yanakwenda vizuri katika kazi za Lifeword nchini China na  Roger na Hilde wamekuwa kiungo muhimu katika kazi.
 Cuba 050509-1 Wakristo wa Cuba wametangaza kuwa mwaka 2009  ni“Mwaka wa Injili”. Wanahitaji maombi ili waweze kufukia watu milioni moja.  
 Congo 060809-1 Omba kwa ajili ya msamaria Purse apate mahitaji kwa ajili ya ukanda wa kiislam wa vita vya mauwaji ya wakristo, ubakaji wanawake, kupeleka watoto vitani na kuuwa yeyote anayetaja ya kuwa Yesu ni Bwana.  
 Mexico 071509-1 Frontier Missions waliopo Hildalgo Coahuila wanahitaji maombi ya fedha ili waweze kuendelea na huduma. Mambo ni magumu. Wamefunguwa karakan ndogo na wanaomba wateja waweze kuja.  
 Mongolia 050409-1 Mmishenary wa Kimarekani aliyoko Mongolia, Tony Crocker, anaomba Mungu afunguwe milango ya kupata wamishenary wa kitaifa katika mkoa wa Kazak huko Mongolia.  
 Nepal 050509-1 Mchungaji  David wa Evangelistic International Ministries anaomba Mungu amruhusu kupanda kanisa kwenye mpaka wa  Nepal na Tibet ambapi itamwezesha kuwahudumia watibeti na wa budha.  
Nepal 050509-3 Ombea mpango wa injili ya nyumba kwa nyumba kwa watu wa  Kamaiyas  ambapo awali walikuwa watumwa, lakini sasa hawana makazi ya kuishi, chakula, madawa na elimu. Huu mkakati utafanyika wiki ya tatu ya mwezi wa saba.  
Nepal 071509-1 Mchungaji David wa Evangelistic International  Ministriesanamba msaada wa fedha wa muda mrefu kw ajili ya kuwahudumia watoto katika maeneo mbalimbali ya Nepal.  Anahitaji kusambaza mabegi ya shule, vitabu, na Maandiko.  
Nepal 092209-1 Mmishenary anaomba apate visa. Maandalizi na serikali yameshaanza, omba visa ipatikane katika muda muafaka bila rushwa kwa wahusika na ikamilike kabla ya tarehe 10.Octoba. Computa yake inahitaji matengenezo. Omba itengenezwe au itumwe mpya kwake. Pia amepoteza kadi yake ya benki, inayomwezesha kuchukuwa fedha za huduma.  
Pakistan 042209-1 Omba kwa ajili ya fedha za msaada wa kusambaza chakula, mablanketi, na madawa kwa wakristo waliokuwa wametekwa na kuumizwa tarehe 22. April.2009 huko Karachi Pakistan.  Wakristo walianza kutekwa mnamo 01.Julai.2009 katika kijiji cha  BahmaniWala Pakistan na makazi mengi na maisha ya watu yamepotea. Mahitaji ya msaada wa dharura yanahitajika kwa haraka. Tarehe 01.May.09 Dola 2000 zilipokelewa kwa msaada, lakini bado zinahitajika zaidi.
Romania 100509-1 Lifeword Broadcast Ministries inaomba kwa ajili ya kuanza huduma ya  utangazaji katika nchi za  Romania na Albania kuwafikia watu wa kabila la Gypsy. Wanategemea kuanza rasmi tarehe19. December. Omba kwa ajili ya viongozi, Bogdan na Daniela Bilav. Fundi mitambo wa Lifeword , David na Daniel Olcean, na Roma (Gypsy) viongozi ambao wata hudumu na kutoa taarifa na mziki kwa dakika 30 kila wiki. Oba kwa ajili ya mpango wa kupanda makanisa na pia fedha zipatikane ili kuweza “kufikia watu wengi zaidi” omba kwa ajili ya roho milioni 10 zilizopotea za wa Gypsy wi kiroma waweze kusikia na kuamini.  
Urusi 042309-1 Omba kwa ajili ya fedha za  "School of Life Piloting", ambazo husaidia kufundisha na kuendeleza busara za kiroho, na uthibiti wa msukumo wa kimwili, na mafunzo ya maisha kwa vijana yatima ambao wamefikia kuondoka katika nyumba ya yatima na kuingia katika ulimwengu ambao ni hatari. Utafiti unaonyesha 90% wanakwenda kuishia jela na kwenye ukahaba. Tanataka kuwabadilisha na wawe na msingi imara wa kristo. Bwana asifiwe, yale mahitaji ya kuendesha huduma kwa mwakamwingine  yamepatikana.
Urusi 042309-2 Omba kwa ajili ya  Andrey Govorov, Sergey Kabanov, Oleg Pirogov na Uyry Furmanov  ambao wanaendesha mafunzo  ya Bibilia kwa wafungwa wa Kursk. Wanaomba Mungu awasaidie wale ambao wamewafikishia injili wapate kazi mara watakapotoka kifungoni.  
Urusi 042309-3 Igor Petrov anaomba Mungu aendelee kubariki  ChristianVideo Courses Ministry.  Haswa anaomba aweze kusogea zaidi na kuwafikia Urusi, Ujerumani,  Ukraine, Israel, Amerika, Australia, Amerika ya kusini na na kwa waongea kirusi ulimwenguni kote.  
Urusi 042309-4 Svetlana Petrov anaomba nguvu za Mungu na fedha ili kuweza kuhudumia nyumba za kutunza wasiojiweza zilizotelekezwa huko Kursk Urusi.  
Urusi 072309-1 Omba milango ya ya injili iwe wazi kwa summer camp 7 za vijana (50-85 kwa lila mtoto , na 70%+ wametoka familia zisizo za kikristo na 4 yatima) katika maeneo ya Kursk Urusi. Pia moto wa wa upendo wa Mungu uamshe mioyo ya watoto wengi.  
Urusi 100509-1 Ndugu Andrey ambaye ni mchungaji wa kanisa la Gypsy anahitaji gari la kanisa lifanyiwe ukarabati. Mahitaji ni dola 2000 kwa ajili ya kukarabati engine, , transmission, na gurudumu mapya.  
Sri Lanka 042709-1 Mchapishaji wa kikristo anayefanya kazi Sir Lanka anaomba Mungu ateue mtu wa kupitisha vipeperushi vya injili katika geti la mwisho la ukaguzi. Kuna kama wafanyakazi 6 wanapata Biblia kwa kwa ajili ya kuwafikia wakimbizi 200,000.  Milango imefunguka na wat wanaokoka.
Marekani 010109-1 Christ Centered Prayer inaomba  Mungu aongeze watafsiri wa lugha tofauti katika tovuti ya maombi ya ulimwengu:  www.ccprayer.org Mpaka sasa Mungu ameshatupatia mtafsiri wa Kiingereza, Kireno, Kirusi, Kispanyiola na Kiswahili.
Marekani 020109-1 Kanisa la Centro De Vida lililoko Atlanta Texas, linaomba Mungu afunguwe milango kwa wafanya kazi waweze kuwafikia watu wenye asili ya kispanyiola. Sikukuu ya Tall Pines huko Atlanta Texas tarehe  04.Oct.09 imeleta mawasiliano na jamii ya watu wa kispanyiola. Ombea mioyo yao imjeukie Mungu mara watakapo tembelewa.
Marekani 051809-1 Ndugu. Joe Brown,mkurugenzi wa  Christ Centered Prayer, alikuwa amelazwa hospitali tarehe 17/May/08 na akagundulika kuwa na  Congestive Heart Failure. Aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya yake kuwa njema, lakini sasa anasumbuliwa na  anemia, blood pressure, and matatizo ya thyroid. Omba watabibu wa afya wampatie matibabu mazuri. Tarehe 30. Set.09 Ndugu Joe alikuwa amelazwa ICU bado anamatatizo makubwa.
Zambia 112408-1 Mmishenar aliyeko Zambia Joseph Mbange anaomba mke wake apokee uponyaji kamili wa malaria.  Bwana asifiwe!  Alice amepona kabisa sasa.
Zambia 112408-2 Pia wanamahitaji ya  $3,000 kwa ajili ya kumaliza kulipia kiwanja chao  na dola 14000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na kupatiwa kupata fedha za matumizi ya kila mwezi, dola 600. Joseph' ameongezewa mapato yake na wafadhili kufikia $600/ kwa mwezi sasa wanahitaji fedha za ujenzi wa nyumba. Mpaka sasa wameshapokea dola 300 kuelekea katika lengo lao.
Zambia 050609-2 Ombea AWANA Zambia's 2009 katika lengo lao la kifikia nasi 6,500 ziokolewe. Na kuanzisha makanisa 50 chini ya mpango wa  AWANA . Bwana asifiwe!, lengo la 6,500 limepitiliza na kufikia nafsi  10,790 na kuanzisha makanisa mapya166 chini ya mpango wa  AWANA.